Adier Palmer   (𝕃𝕦𝕓𝕒𝕟𝕘𝕒)
137 Followers · 101 Following

I was born to write experiences and feelings
Joined 8 February 2018


I was born to write experiences and feelings
Joined 8 February 2018
YESTERDAY AT 10:36

Eksi Wangu!


Wa kwanza mwenye kiburi, hakujua jina pole,
Na zaidi mwenye siri, na uongo mwingi tele,
Msichana wa Kinyeri, mfupi mwenye kelele,
Ni EX wangu wa kwanza, kwa mwaka tukaachana!

Wa pili ni msomali, wa kutoka Somalia,
Hakupenda za halali pesa aliniibia,
Zikawa yake nauli, Somali akakimbia,
Huyo kwa kusema kweli, figa namkumbukia,

Wa tatu alinichoma,nkwa hayo yake madai,
Ati nina kiserema, sina jembe bwana wai?
Akapata mkulima, wakahamia Kitui,
Kwa wote aliniuma, mwenzako humuumbui!

Nikalitafuta toto, lilo Kenyatta chuoni,
Hili lilikuwa moto, watoto usitamani,
Nina miwili mikato, makovu yalo mwilini,
Ningerushwa hata mto, Kenyatta bewa mjini!

Wa mwisho mwanasiasa, mbaya kama Zakayo,
Hakujua sina pesa, vya ghali vyake vileyo,
Hakika alinitesa,.akenda na wenye vyeyo,
Nimekoga hivi sasa, nenda soko mbiyo mbiyo,

Anipa nile limau, na huku nina papai,
Vipi amenisahau, kula vichachu sijui,
Sili mimi kaukau, na vyororo sibagui,
Ni heri nife kwa kiu, ela sinywi chapwa chai!


|Dear_eksi|

-


3 MAY AT 12:13

Sasa mbona unanipa jeraha
Pindi unamwaga sera
Mpaka nikaunga tela
Haukuwaga hivi
Maisha yangu umeyajaza karaha
Yaani umeyachange colour
Nikisema unasema ninakera
Haukuwaga hivi
Mashundu umeyajaza kwa dera
Kila mara kunipokonya hela
Ama unataka kunisukuma jela
Haukuwaga hivi
Nakumbuka tulianza na love "hera"
Kuapa tungependana mpaka ahera
Na sahi unanitusi kichwa mapera
Haukuwaga hivi

|Haukuwaga hivi|

-


3 MAY AT 12:13

Sasa mbona unanipa jeraha
Pindi unamwaga sera
Mpaka nikaunga tela
Haukuwaga hivi
Maisha yangu umeyajaza karaha
Yaani umeyachange colour
Nikisema unasema ninakera
Haukuwaga hivi
Mashundu umeyajaza kwa dera
Kila mara kunipokonya hela
Ama unataka kunisukuma jela
Haukuwaga hivi
Nakumbuka tulianza na love "hera"
Kuapa tungependana mpaka ahera
Na sahi unanitusi kichwa mapera
Haukuwaga hivi

|Haukuwaga hivi|

-


3 MAY AT 12:11

Sasa mbona unanipa jeraha
Pindi unamwaga sera
Mpaka nikaunga tela
Haukuwaga hivi
Maisha yangu umeyajaza karaha
Yaani umeyachange colour
Nikisema unasema ninakera
Haukuwaga hivi
Mashundu umeyajaza kwa dera
Kila mara kunipokonya hela
Ama unataka kunisukuma jela
Haukuwaga hivi
Nakumbuka tulianza na love "hera"
Kuapa tungependana mpaka ahera
Na sahi unanitusi kichwa mapera
Haukuwaga hivi

|Haukuwaga hivi|

-


31 MAR AT 10:20

Sabalkheri wangwana, Lubanga nawasalimu,
Ninaomba kusemana, nanyi wapendwa walimu,
Nimechoka kutengana, na wapoa muhimu,
Wapi chuo cha mapenzi, nami pia nihitimu?

Kama elimu maisha, mapenzi nayo ni nini?
Kama mapenzi huisha, mbona mimi siamini?
Iwapo kunafundisha,basi upo mtihani?
Wapi chuo cha mapenzi, nami pia nihitimu?

Kakamega sijaona, wafunzapo hiyo kozi,
Ambira hadi Nangina, sijaona hiyo kozi,
Sijui ipo Botswana, nafsi angu chokozi,
Wapi chuo cha mapenzi, nami pia nihitimu!

Kwahitaji daftari, vifutio na kalamu,
Kuna walimu hatari, wasifanye ninywe sumu,
Kwataka niwe ngangari, je, mitihani ni ngumu?
Wapi chuo cha mapenzi, nami pia nihitimu?

Huko pia kuna labu, vifaa vipi vilimo,
Wanafunza 'malakabu', majina yenye vipimo,
Tagawa huko vitabu, lugha ya mapenzi imo?
Wapi chuo cha mapenzi, nami pia nihitimu?

Nahitaji lugha yao, mademu walo warembo,
Na niwe mkaliwao, wajuwe natoka ng'ambo,
Waniite baba lao, nizidishe majigambo,
Wapi chuo cha mapenzi,nami pia nihitimu?

Swali langu nijibuni, Adiba nitaridhika,
Limekwama akilini, kitwani limejitwika,
Limezidi mawazoni, ndyo'mana nimeandika,
Wapi chuo cha mapenzi, nami pia nihitimu?


|Wapi chuo cha mapenzi|

-


15 MAR AT 16:58

A polite notice to anyone
wishing to block me this year.

Kindly make sure it's
IRREVERSIBLE.


If you can't stand my negatives
Don't stand my positives also.
If you can do a day without me
Make it a lifetime decision too.
Life must continue...

It's time to unhung me
from your horrible life

|2024|


-


8 MAR AT 9:22

One thing personally najua
Ni that our love ni maua
Na hakuna kitu kitayaua
Leave alone kukuchukua

It's so deep, doo haziwezi nunua
Na kwa madem soo bado nitakuchagua
Heri nipoteze rada kama Gachagua
Juu wakileta noma, maneno nitafyatua

Halafu sahi nikama nishajua
Hii yote ni Mungu amejibu dua
Siamini ati ni mimi ushaamua

Sitaki mchanga uingie kwa kitumbua
Kama vile ilimess love ya Wambua na Kambua
Kwa hizo deepfaked videos akimnyandu***

Babe, I know kuna day hii love itakua
So sweeter than avocado na muwa
Na tena perfect, juu rohoni ushatua

We're here to stay, hiyo niko sure
Hata kama itamean kuishi kwa mashua
Juu kwa jangwa langu wewe ndio mvua
Hiyo tena ninaswear, nikisema niko sure
Kama bet, nimerisk juu najua niko sure


|4-U|

-


20 FEB AT 18:22

ANA DAMU YA KUNGUNI

Jiulize ni kwa nini,uanzapo kuongea,
Sana sana makundini,watu hukuondokea,
Ndugu ujitathmini,hakika umepotea,
Sisi tuwakuombea,mwenye damu ya kunguni!

Mwenye damu yakunguni,nayo Lugha ya ajuza,
Wengi hawamtamani,maneno yake yaliza,
Yeye ana walakini,dosari kuliko pweza,
Kama wewe umefunza,sote hutuona duni!

Sote hutuona duni,na hilo tumezowea,
Kazi zetu zote guni,yeye tu amebobea,
Umewachokoza mbuni,mateke atapokea,
Sisi tuwakuombea,upae hadi hewani!

Upae hadi hewani,ujione kama bingwa,
Mewashinda gazetini, wandishi kwako wapingwa,
Yeye qwetu mpinzani,metia mipaka tingwa,
Twakwombea mtafiti,hesabu hadi mizani!

Hesabu hadi mizani,utunge kwa kukosoa,
U hodari hesabuni,nasi tushakuzoea,
We nduli kwa majirani,na waja mekutegea,
Kurekebisha hajui,ywatwanika peupeni!

Ywatwanika peupeni,ywajisifu mjuaji,
Amezidi zetu mboni,na amejivunjia mji,
Twamwachia waamuzi,kesi wasome majaji,
Sisi tuwakuombea,sirekebike kidogo!


|Kimelea|

-


8 FEB AT 19:23

Hiliyambo limekithiri,alifanyao haoni,
Nalisema nami si siri,limechacha kanisani,
Naona litanawiri,mapema mlikomeni,
Wanadada walokole,tunzeni waume wenu!

Walalama kilamara,eti nyinyi hamweshimu,
Mwajiletea madhara,na pia mwajihukumu,
Wa kanisa ndi vinara,la waume hamweshimu,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!

Kija kwako mhubiri,kabati walifungua,
Hadi wapanda kwa dari,sahani nzuri watoa,
Mfanyavyo si vizuri,badilisheni tabia,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!

Wanaume wazunika,Kila muda kanisani,
Nyumbani na waboeka,mfanyapo na kuhani,
Nyoyoni wasononeka,boma lao mabadini,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!

Wacha mume kafurahi,muishini kwa neema,
Ndoa yenu tamirihi,mtachekelea wema,
Kitazama tanabahi,mtasifiwa salama,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!

Safari nazo punguza,mrembeshe wako mume,
Najua nimewaguza,mume siye paka shume,
Yeye atauguuza, moyo wako usikwame,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!

Rekebisheni nasihi,ndoa ziache vunjika,
Someni wangu nasihi, mbeleni nawapeleka,
Nasaha Nimewaahi,ndoa na hazitavunjika,
Wanadada walokole, tunzeni waume wenu!


|Wanadada walokole|

-


3 FEB AT 15:00

ATAKUWA MAMA MTU

Nina wangu chautamu,'kiwa naye naridhia
Yeye kwangu ni muhimu,kaniteka kihisia
Kwake hainishi hamu,daima anivutia
Atakuwa mama mtu,nami niwe baba mtu.

Huyu ndo kichaa wangu,napenda wazimu wake
Namuelewa kivyangu,tangu mie aniteke
Sitaki atoke pangu,moyo wangu uteseke
Atakuwa mama mtu,nami niwe baba mtu.

Kwake mie ni mhuni,apenda usela wangu
Nyumbani ndo maskani,pazuri sio pachungu
Kazi yake kijiweni,kuzichana ndevu zangu
Atakuwa mama mtu,nami baba mtu.

Yeye kwangu mhubiri,injili yake yatamba
Kauli zake ni nzuri,haziboeshi zabamba
Kwake hali kweli nzuri,hatujawahi kulumba
Atakuwa mama mtu,nami baba mtu.

Kwake nimekuwa teja,sina mwendo asilani
Kaniteka mwenye tija,niko 'high' jamanini
Hoja ninazoboboja,sizielewi wendani
Atakuwa mama mtu,nami niwe baba mtu.

Kwangu amekuwa mwizi,ameniiba mzima
Na tena mchana wazi,kabla jua kuzama
Aniita laazizi,natoa kutu 'mi chuma
Atakuwa mama mtu,nami niwe baba mtu.

Kwangu amekuwa mama,mtoto nadekadeka
Kutwa ananitazama,nisiweze kudhurika
Hapa kweli nimefuma,ndege simwachi hakika
Atakuwa mama mtu,nami niwe baba mtu.

-


Fetching Adier Palmer Quotes